Tanzania imeendelea na mchakato wa kuwaandikisha wakimbizi wa Burundi waishio nchini humo ili kuwarudisha nyumbani kwa hiyari katika kambi zake za mkoani Kigoma. Mchakato huo unaendelea huku baadhi ya wakimbizi wakiwa hawana utayari wa kurejea nchini mwao.