1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Mbunge Bob Menendez akana madai ya rushwa, asema hajiuzulu

26 Septemba 2023

Mbunge wa chama cha Democratic cha nchini Marekani Bob Menendez amekana mashitaka ya rushwa na kusema karibu dola nusu milioni zilizokutwa nyumbani kwake zilikuwa ni akiba yake na si rushwa.

https://p.dw.com/p/4WnmS
Fedha zilizokutwa nyumbani kwa mbunge Bob Menendez zikiwa zimewekwa kwenye koti lenye jina lake pamoja na bahasha ziliyzkuwa na fedha ndani ya koti hilo
Fedha zilizokutwa nyumbani kwa mbunge Bob Menendez zikiwa zimewekwa kwenye koti lenye jina lake pamoja na bahasha ziliyzkuwa na fedha ndani ya koti hilo Picha: AP Photo/picture alliance

Menendez amesema fedha hizo zilikuwa nyumbani kwa matumizi ya dharura.

Mbunge huyo wa New Jersey anayekabiliwa na ongezeko la miito ya kujiuzulu amesema anaamini atafutiwa madai kwamba alipokea fedha taslimu na dhahabu ili kuwasaidia washirika wa kibiashara wa nchini Misri na New Jersey. 

Menendez amesema fedha hizo zilizokutwa nyumbani kwake Ijumaa iliyopita zilitoka kwenye akaunti zake za akiba aliyojiwekea kutokana na mapato halali kwa zaidi ya miaka 30.

Kulingana na hati ya mashtaka, mamlaka zilikuta karibu bahasha 10 zilizojaa maelfu ya dola zilizokuwa na alama za vidole vya baadhi ya washitakiwa kwenye kesi hiyo.