Kuvunjika kwa amani kumekuwa na mchango mkubwa kwa watu kuyakimbia makazi au nchi zao na kwenda kutafuta hifadhi katika nchi nyingine. Wakimbizi wamekuwa wakiyatafsiri maisha ya ukimbizi kama kuzuizini ambako haki mbalimbali hupungua au kupotea. Hali hii inapelekea wengi wa wakimbizi kupiga kelele juu changamoto zao.