Matatizo ya ardhi kwa jamii ndogo Kenya, yana athari kubwa kijamii, kiuchumi, na kisiasa. Jamii hizi ndogo na asili mara nyingi hukabiliwa na migogoro ya ardhi, upotevu wa rasilimali za ardhi, unyanyasaji na ukiukaji wa haki zao, yote haya ambayo yana athari kubwa kwa maendeleo yao ya kijamii na kiuchumi. Jamii hizi mara nyingi huwa wakulima wadogo, wafugaji, na wawindaji. Msikilize Wakio Mbogho.