Mbio za kuuzungusha mwenge zafanyika salama Australia
24 Aprili 2008Matangazo
CANBERRA
Zoezi la kuuzungusha mwenge wa Olimpiki nchini Australia zimeanza chini ya ulinzi mkali kuzuia ghasia zozote za waandamanaji wanaoipinga China.Maafisa nchini humo wamesema kiasi cha watu saba wamekamatwa kwenye ghasia na maandamano madogo yaliyofanyika kabla ya kuanza kwa mbio hizo za mwenge katika mji mkuu Canberra.Watu waliokuwa wamebeba bendera za China na Tibet ni miongoni mwa waandamaji ambao wamekusanyika katika mabustani yaliyoko kwenye eneo la kupitishiwa mwenge huo.Mwenge wa Olimpiki ambao utarudi Beijing kwa ajili ya sherehe za ufunguzi wa michezo ya Olimpiki mwezi Agosti,umekuwa ukiiangaziwa katika kipindi cha wiki kadhaa sasa kutokana na maandamano na ghasia dhidi ya utawala wa China katika jimbo la Tibet.