1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mazungumzo ya kusitisha mapigano Gaza yaingia siku ya pili

16 Agosti 2024

Wapatanishi wa kimataifa wanaofanya mazungumzo ya kusitisha mapigano katika ukanda wa Gaza wanakutana kwa siku ya pili leo mjini Doha, Qatar.

https://p.dw.com/p/4jXW4
Israel Grenze Gazastreifen | Israelische Panzer
Picha: Amir Cohen/REUTERS

Hayo yanatokea huku wanadiplomasia wakuu wa Ulaya wakitarajiwa kuelekea Israel kwa lengo la kusisitiza umuhimu wa kufikia makubaliano ya kusitisha vita na kutotanua mzozo huo.

Msemaji wa Baraza la Usalama la Taifa la Marekani, John Kirby, amesema kuwa mazungumzo ya Doha yamekuwa na kile alichokiita "mwanzo mzuri" japo amekiri kuna kazi kubwa ya kufanywa.

Duru mpya ya mazungumzo ya kusitisha mapigano Gaza imeanza mjini Doha jana Alhamisi bila ya uwepo wa kundi la Hamas, ambalo limeishutumu Israel kwa kuongeza masharti zaidi kwenye mapendekezo ya awali yaliyokubaliwa na Hamas.