1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mazungumzo ya amani ya Sudan kuanza tena Uswisi

14 Agosti 2024

Mazungumzo kuhusu mapigano ya nchini Sudan yataanza tena katika mji wa Geneva nchini Uswisi. Majadiliano hayo yatazingatia juu ya kufikishwa misaada kwa mamilioni ya watu wanaokabiliwa na njaa

https://p.dw.com/p/4jRok
Abdul Fattah Al-Burhan na Mohamed Hamdan Dagalo
Jenerali Mkuu wa jeshi la Sudan Abdul Fattah Al Burhan na Mohammed Hamdan Dagalo kiongozi wa kundi la wanamgambo la RSF Picha: Bandar Algaloud/Mahmoud Hjaj/AA/picture alliance

Marekani imezialika pande zote mbili zinazopigana kwenye mazungumzo hayo ingawa kwa sababu za kiusalama eneo hasa yatakapofanyika mazungumzo hayo katika jiji la Geneva halikutajwa.

Marekani kuanzisha mazungumzo ya amani ya Sudan, licha ya jeshi kutothibitisha

Vita vimeendelea nchini Sudan tangu mwezi Aprili mwaka 2023, kati ya jeshi la Sudan na wanamgambo wa RSF.

Mapigano hayo yamewakosesha makazi zaidi ya watu milioni 10 nchini humo na wengine wameikimbia nchi na kuvuka mipaka. Kulingana na Umoja wa Mataifa, pande zote mbili kwenye mzozo huo zinazuia misafara ya misaada kuwafikia wanaoihitaji.