1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mazungumzo ya mzozo wa Nagorno-Karabakh yafikia hatua chanya

21 Septemba 2023

Armenia imesema haipo kwenye harakati zozote za kuwahamisha raia kutoka Nagorno-Karabakh, baada ya Azerbaijan kudai mapema leo kuchukua udhibiti kamili wa eneo hilo linalozozaniwa.

https://p.dw.com/p/4Wf6z
Aserbaidschan | Ankunft der Armenischen Delegation zu Gesprächen in Yevlakh
Picha: REUTERS

Waziri Mkuu wa Armenia Nikol Pashinyan amesema katika taarifa kwamba ana imani, haki ya Waarmenia wa Nagorno-Karabakh ya kuishi katika nyumba zao kwa usalama na heshima itazingatiwa.

Kwa upande wake, Azerbaijan imesema kuwa mazungumzo ya kusuluhisha mzozo huo yalikuwa na matokeo chanya, na wamefikia makubaliano ya kukutana tena siku za usoni.

Mustakabali wa Nagorno Karabakh wajadiliwa

Ofisi ya rais wa Azerbaijan imesema serikali ya Baku imekubali kupeleka chakula, mafuta na misaada ya kibinaadamu katika eneo hilo.