1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mazungumzo kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran kufanyika Jumamosi mjini Paris

29 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CUPG

Wajumbe wa mataifa sita yanayojaribu kuzuia mpango wa nyuklia wa Iran watakutana mjini Paris Ufaransa Jumamsoi ijayo.

Msemaji wa wizara ya mambo ya kigeni nchini Uingereza, Kim Howells, amesema mkutano huo utakaozijumulisha nchi tano wanachama wa kudumu wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, zikiwemo, China, Ufaransa, Urusi, Marekani na Uingereza, pamoja na Ujerumani, utafanyika siku moja baada ya mazungumzo kati ya mratibu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya, Javier Solana, na mpatansihi wa Iran katika mzozo wa nyuklia, Saeed Jalili.

Iran imesema itawasilisha mapendekezo mapya katika mkutano na Solana siku ya Ijumaa lakini ikasema haitasisitisha shughuli ya kurutubisha madini ya uranium kama inavyotakiwa na Umoja wa Mataifa.