1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mazungumzo kati ya Mike Pence na Donald Tusk Magazetini

Oumilkheir Hamidou
21 Februari 2017

Mazungumzo kati ya makamo wa rais wa Marekani Mike Pence na Donald Tusk mjini Brussels, Martin Schulz na mageuzi ya Agenda 2010 na uwezekano wa kusikilizwa simu za mkononi za wakimbizi ni miongoni mwa mada magazetini.

https://p.dw.com/p/2XxbJ
EU - USA Mike Pence & Donald Tusk in Brüssel
Picha: picture-alliance/AP Photo/T. Monasse

 

Tunaanzia Brussels ambako makamo wa rais wa Marekani Mike Pence alimalizia ziara yake ya Ulaya kwa kuzungumza na mwenyekiti wa baraza la Umoja wa ulaya Donald Tusk. Gazeti la mjini Freiburg "Badische Zeitung" linaandika: " Mwenyekiti wa baraza la Umoja wa Ulaya Donald Tusk machozi yalikuwa yakimlenga lenga baada ya kukutana na Mike Pence na kukutana baadae kwa pamoja na waandishi habari akisema " wao wote walikuwa wakitegemea kwa hamu kubwa kukutana."Wao wote? Ndo kusema , ulaya nzima ilikuwa na hamu ya ziara ya mfuasi huyo anaefuata msimamo mkali wa kihafidhina ambae nadharia ya mabadiliko kwake yeye ni sehemu tu  ya "ukweli mbadala" na ambae kutoka kwa mkubwa wake, Donald Trump hakuwa na jengine isipokua "salam za kijuu juu? Bara kongwe la Ulaya linastahili bora zaidi kuliko hayo."

Schulz aahidi mageuzi ya Ajenda 2010

Chama kidogo katika serikali kuu ya muungano mjini Berlin, Social Democrat, kinazidi kujivunia imani ya wapiga kura tangu Martin Schulz alipochaguliwa kugombea kiti cha kansela. Na tangu wakati huo spika huyo wa zamani wa bunge la ulaya anafafanua malengo yake. Hivi karibuni anasema akichaguliwa kuwa kansela ataifanyia marekebisho ajenga 2010. Gazeti la "Neue Osnabrücker Zeitung" linaandika: "Anataka ifanyiwe marekebisho ajenda 2010. Na Martin Schulz hajakosea. Kwasababu hakuna kilichoiathiri zaidi SPD katika kipindi cha mwongo mmoja uliopita kama mageuzi ya Agenda 2010. Yalimgharimu wadhifa wake kansela wa zamani Gerhard Schröder kwasababu tija ya mageuzi hayo ilikawia kujitokeza. Ingawa ilidhihirika baadae na kuifadisha nchi nzima. Ishara kwamba ukosefu wa ajira unaweza kudhibitiwa ni miongoni mwa matunda ya ajenda 2010 na kila upande unayatambua. Hata hivyo mabadiliko yanawezekana . Lakini kwa kuzingatia mada zote mbili: Muda wa malipo ya wasiokuwa na ajira na maendeleo katika soko la ajira ni mambo ambayo hayawezi kutangana. Anaetaka kurefusha upande mmoja tu, aajue ataudhoofisha wa pili."

Simu za mkononi wa wanaoomba kinga ya ukimbizi huenda zikasikilizwa

Mada yetu ya mwisho magazetini inahusu mpango wa serikali kuu wa kuchunguzwa simu za mkononi za wenye kuomba kinga ya ukimbizi na ambao hawataki kushirikiana na maafisa wa serikali. Gazeti la "Allgemeine Zeitung" linaandika: "Ni kuingilia mambo ya ndani ya mtu" anasema mkuu wa chama cha siasa kali za mrengo wa kushoto, die Linke, Katja Kipping. Na hajakosea. Hata hivyo kitendo hicho kinavumilika. Kwasababu kinawahusu watu wanaoomba hifadhi nchini Ujerumani, wanaolipwa huduma za jamii lakini vitambulisho vyao hawataki kuvionyesha. Anaejikuta katika hali kama hiyo anabidi lakini ashirikiane na maafisa wa serikali ,na ikilazimika basi kwa kuruhusu uchunguzi kama huo ufanyike.

Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/Inlandspresse

Mhariri. Mohammed Abdul-Rahman