Mawaziri wanne wapya nchini Somalia watangaza kujiuzulu
4 Desemba 2007Matangazo
BAIDOA.Mawaziri wanne katika serikali mpya ya mpito nchini Somalia wametangaza kujiuzulu siku moja tu baada ya kuapishwa, likiwa ni pigo la kwanza kisiasa kwa Waziri Mkuu mpya Nur Hassan Hussein.
Mawaziri hao waliyotangaza kujiuzulu ni wa mambo ya ndani Hassan Mohammed Nur , waziri wa biashara Abdikafi Hassan, waziri wa maridhiano Sheikh Aden Maden na waziri wa mipango Ibrahim Mohammed Isaq.
Akizungumza kwa niaba ya wenzake Hassan Mohammed Nur ambaye ni mbabe wa zamani wa kivita amesema kuwa kujiuzulu kwao kunatokana na kutoshauriwa kabla ya kuteuliwa.
Wakati huo huo watu watano wameuawa mjini Mogadishu na wengine watatu katika mji wa Jowhar mnamo wakati ambapo hali ya umwagaji damu ikizidi katika nchi hiyo ya pembe ya afrika.