1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Viongozi wa Uingereza, Ireland wazuru serikali ya Belfast

5 Februari 2024

Viongozi wa Uingereza na Ireland leo Jumatatu wamekwenda mjini Belfast,Ireland ya Kaskazini,kukutana na serikali mpya ya jimbo hilo iliyoingizwa madarakani baada ya kumalizika kwa miaka miwili ya mgogoro wa kisiasa.

https://p.dw.com/p/4c4JX
 Belfast 2024 | Michelle O'Neill
Kiongozi wa Ireland Kaskazini Michelle O'Neill kutoka chama cha Sinn Fein.Picha: Liam McBurney/AP/picture alliance

Viongozi wa Uingereza na Ireland leo Jumatatu wamekwenda mjini Belfast,Ireland ya Kaskazini,kukutana na serikali mpya ya jimbo hilo iliyoingizwa madarakani baada ya kumalizika kwa miaka miwili ya mgogoro wa kisiasa.

Soma: Chama cha DUP yaridhia kurejea serikali ya Ireland Kaskazini

Serikali mpya ya kugawana madaraka ya Ireland Kaskazini wiliteuliwa siku ya Jumamosi na bunge la jimbo hilo ambalo ni sehemu ya Uingereza. Waziri mkuu wa Uingereza Rishi Sunak na mwenzake wa Ireland Leo Varadkar  wameitembelea serikali hiyo mpya katika kasri la Stormont mjini Belfast wakati ikikutana kwa mara ya kwanza tangu ilipoteuliwa.

Serikali hiyo mpya ya Ireland Kaskazini inaongozwa na waziri kiongozi  Michelle O'Neill kutoka chama cha Sinn Fein.Serikali ya mjini London imekubali kuipatia Ireland Kaskazini zaidi ya pauni bilioni 3 kama sehemu ya fedha za kuisadia serikali hiyo mpya.

 

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW