Mawaziri wa EU waridhia kuleta mageuzi ya sheria za madeni
21 Desemba 2023Matangazo
Mageuzi hayo yatazipa nchi za Umoja huo zenye madeni makubwa, muda wa kutosha wa kupunguza nakisi na pia yatazipa wigo mpana zaidi wa kuwekeza.
Mnamo miaka ya karibuni madeni yalifikia viwango vya kuvunja rekodi katika nchi hizo, kutokana na janga corona na pia kutokana na juhudi za kupambana na bei za juu za nishati zilizosababishwa na vita vya Ukraine.
Waziri wa fedha wa Uholanzi Sigrid Kaag, amesema pana motisha ya kuleta mageuzi na fursa ya kuwekeza.
Amesema sheria husika zitawekwa kwa usahihi zaidi kulingana na mahitaji.