Mawaziri wa Nje wa NATO wakutana
3 Desemba 2009Mawaziri hao watajadili hasa njia za kuliimarisha jeshi la kimataifa -ISAF nchini Afghanistan na juu ya kuwaingiza wanachama wapya.
Katibu mkuu wa mfungamano wa kijeshi wa nato Anders Fogh Rasmussen alisafiri sana katika wiki zilizopita.
Lengo la ziara alizofanya lilikuwa kuzishawishi nchi wanachama wa nato zitoe askari zaidi ili kuliimarisha jeshi la kimataifa ,linaloongozwa na nato nchini Afghanistan.
Kabla ya kuanza mkutano wa leo wa mawaziri wa mambo ya nje wa nchi za NATO mjini, Brussels katibu mkuu Rasmussen alisisitiza kwamba vita vya nchini Afgnaistan siyo jukumu la Marekani pekee yake.
´´Vita hivi siyo vya Marekani peke yake. Yanayotokea nchini Afghanistan
yanawahatarisha dhihiri wananchi katika nchi zetu zote"
Katibu mkuu huyo amesema ni kutokana na hatari inayotokea Afghanistan kwamba ni lazima kuliimarisha jeshi la kimataifa linaoongozwa na nato nchini Afghanistan ISAF kwa kuongeza idadi ya askari.
Marekani imeamua kupeleka wanajeshi alfu 30 zaidi nchini Afghanistan ili kuimarisha harakati za kupambana na magaidi wa alkaida na wapinzani wa kitaliban.
Katibu mkuu wa NATO bwana Rasmussen amesema amehakishiwa kupata askarri alfu tano zaidi kutoka wanachama wengine wa nato.
Kwa mujibu wa duru za kidiplomasia, Georgia imeahidi kuongeza wanajeshi mia 770 na Uturuki imeahidi askari 800 zaidi kwa ajili ya Afghanistan na Poland imethibitisha kwamba itatoa askari wengine 600.
UJERUMANI
Lakini Ujerumani bado haijakuwa tayari kutekeleza maombi ya kuongeza askari wake nchini Afghanistan.
Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Guido Westerwelle ameeleza kwa nini.
´´Kwanza inahusu malengo na mikakati. Na ndipo baada ya hapo vipatikane vifaa vya kutuwezesha kufikia malengo hayo .Mjadala uliopo nchini mwetu unaogusia tu suala la askari wangapi wanaopaswa kupelekwa; mjadala kama huo tunaupinga."
Kwenye mkutano woa wa leo mjini Brussels mawaziri wa mambo ya nje
wa chi za nato pia watajadii suala la kuupanua mfungamano wao. Pamoja
na mengine wataamua iwapo Montenegro na Bosnia Herzegovina
zitaingizwa kwanza katika hatua ya kwanza ya kuelekea kwenye
uanachama.
Mwandishi /Birgit Schmeitner//ZA
Imetasfiriwa na /Mtullya Abdu.
Mhariri/Hamidou Oummilkheir