Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Ulaya wataka taifa la Palestina
22 Januari 2024Matangazo
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Stephane Sejourne amewaambia waandishi wa habari kwamba maazimio ya Netanyahu yanatia wasiwasi na kuna umuhimu wa Taifa la Palestina kuhakikishiwa usalama.
Ubelgiji, ambayo ni rais wa sasa wa Umoja huo, kupitia Waziri wake Hadja Lahbib, imesema hali katika Ukanda wa Gaza ni ya dharura kutokana na kitisho cha njaa na majanga na kutaka mapigano kusitishwa pamoja na mateka kuachiliwa huru.
Mawaziri hao wanakutana mjini Brussels kujadiliana mzozo wa Gaza.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel, Israel Katz, pia anahudhuria.