Mawaziri wa mambo ya nje wa NATO kukutana
29 Novemba 2022Wito huo unatarajiwa kutolewa katika mkutano utakaofanyika leo na kesho Jumatano. Kadhalika wito huo unakuja baada ya rais wa Ukraine kuwaambia wananchi wake kutarajia wiki nyingine ya baridi na kiza kufuatia mashambulizi yaliyofanywa na Urusi dhidi ya miundo mbinu ya Ukraine.
Mawaziri wa mambo ya nje wa Jumuiya ya NATO watakaokutana mjini Bucharest, nchini Romania watajikita kuzungumzia hatua ya kuongeza msaada wa kijeshi kwa Ukraine ikiwemo mifumo ya ulinzi wa anga pamoja na silaha pamoja na msaada usiokuwa wa kijeshi kama mafuta, vifaa tiba, na vifaa vinavyotumika wakati wa baridi kali.
Ujerumani ambayo hivi sasa inashikilia uongozi wa kundi la nchi tajiri kiviwanda duniani,G7 nayo inapanga mkutano na baadhi ya washirika wa kundi hilo pembezoni mwa mkutano huo wa NATO wakati ikijaribu kushinikiza hatua za kuharakisha ujenzi mpya wa miundo mbinu ya nishati ya Ukraine.