1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaLuxembourg

Mawaziri wa mambo ya nje wa EU wakutana Brussels

26 Juni 2023

Mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya watakutana huko Luxembourg kujadili masuala mbali mbali huku tukio la uasi wa kundi la Wagner nchini Urusi likitarajiwa kugubika kikao hicho

https://p.dw.com/p/4T3iR
Luxembourg EU-Minister Migrationsabkommen
Picha: RTRTV

Mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya watakutana leo huko Luxembourg kujadili masuala mbali mbali huku tukio la uasi wa kundi la Wagner nchini Urusi likitarajiwa kugubika kikao hicho.

Soma pia: Urusi baada ya kitisho cha uasi

Mwanadiplomasia wa ngazi ya juu katika Umoja huo Joseph Borrell amefanya mashauriano na baadhi ya viongozi wenzake mwishoni mwa juma wakati wapiganaji wa Wagner walipokuwa wakiusogelea mji mkuu wa Urusi Moscow, kwa lengo la kutaka kuuangusha uongozi wa kijeshi nchini humo.

Mkutano wa Luxembourg utahudhuriwa pia na waziri wa mambo ya nje wa Ukraine, Dmytro Kuleba kwa njia ya video. Mawaziri hao wanatarajiwa kuonesha mshikamano na Ukraine na kutangaza mipango ya kuipelekea makombora milioni 1 nchi hiyo. Aidha mawaziri hao pia watajadili kuhusu mgogoro kati ya Serbia na Kosovo.