Mawaziri wa mambo ya nje wa EU wajiandaa kuijadili Sudan
22 Mei 2023Siku ya Jumapili, mashambulizi ya anga,ufyetulianaji risasi uliendelea kushuhudiwa katika mji mkuu Khartoum kabla ya kutangazwa makubaliano hayo.
Usitishaji mapigano unatarajiwa kutowa nafasi ya kupelekwa msaada wa kibinadamu kwa raia nchini humo na unatarajiwa kuanza baadae leo Jumatatu kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Marekani na Saudi Arabia,Jumamosi Jioni kufuatia mazungumzo yaliyofanyika Jeddah.
Soma pia: Nchi zenyeushawishi zatakiwa kusuluhisha mzozo wa Sudan
Nchi hizo mbili kwenye taarifa yao ya pamoja zilikiri juu ya kukiukwa kwa makubaliano ya awali lakini zikasema makubaliano ya safari hii ni tofauti. Umoja wa Afrika,Umoja wa Mataifa na jumuiya ya ushirikiano wa kiserikali wa nchi za mashariki mwa Afrika IGAD zimeyapongeza makubaliano hayo.