1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mawaziri wa fedha wa Ulaya na wataalamu wa uchumi wakutana mjini Paris

18 Januari 2008
https://p.dw.com/p/CuGq

Mawaziri wa fedha na maafisa wa uchumi kutoka Uingereza, Ujerumani, Ufaransa na Italy wamekutana mjini Paris Ufaransa kujadili mkakati wa pamoja wa Ulaya kukabilian ana kuyumba kwa masoko ya fedha.

Mazungumzo hayo yanafanyika wakti kukiwa na wasiwasi wa athari za mikopo ya majumba nchini Marekani, ambazo zimeyavuruga masoko ya fedha tangu mwaka jana.

Akizungumza kwenye mkutano huo wa mjini Paris, kamishna wa Umoja wa Ulaya anayehusika na maswala ya uchumi, Joaquin Almunia, amesisitiza kwamba mpango wa kifedha wa Marekani unaotarajiwa utasaidia masoko ya Ulaya.

Hata hivyo maafisa wa Ulaya wansema changamoto kubwa ni kufikia makubaliano ya njia za kuongeza uwazi katika masoko na katika sekta ya benki.