Mawaziri wa fedha wa nchi nne za Ulaya wakutana kujadili sokomoko la sekta ya fedha
18 Januari 2008Matangazo
PARIS:
Mawaziri wa fedha kutoka Uingereza,Ujerumani,Ufaransa na Italia wamekutana mjini Paris kujadili mkakati wa pamoja wa jinsi ya kukabiliana na misukosuko katika sekta ya fedha.Waziri wa fedha wa Ufaransa-Christine Lagarde-amekuwa mwenyeji wa mkutano huo huku wasiwasi ambao uliitikisa soko la fedha tangu mwaka jana kutokana na mgogoro wa mikopo ya nyumba wa Marekani,ukiwa unaongezeka. Maafisa wanasema changamoto kubwa kwa nchi nne za Ulaya ni kufikia muafaka kuhusu mbinu gani za kutumiwa ili kuzidisha uwazi katika sekta za benki pamoja na masoko.