Mawaziri wa Armenia na Azerbaijan kukutana Washington
10 Julai 2024Matangazo
Tangazo la mkutano huo limetolewa na msemaji wa wizara ya mambo ya nchi za nje wa Armenia na kuthibitishwa na ofisi ya waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani.
Nchi hizo mbili jirani zimepigana vita mara mbili kuwania jimbo lililojitenga la Azerbaijan la Nagorno Karabakh ambalo lilikuwa na wakaazi wengi wenye asili ya Armenia. Mwaka jana Azerbaijanilichukua udhibiti wa jimbo katika operesheni yake ya siku moja na kuwalazimisha zaidi ya Armenia 100,000 kulikimbia.
Juhudi za upatanishi za miaka mingi zimeshindwa kumaliza mivutano ya nchi hizo lakini viongozi wake wameashiria miezi ya hivi karibuni kwamba mkataba wa amani uko mbioni kupatikana.