Mauritania yafuzu kucheza fainali za AFCON
19 Novemba 2018Barani Afrika mauritania imefuzu kucheza katika fainali za kombe la mataifa ya Afrika jana Jumapili wakati walipoishinda Botswana na kunyakua nafasi katika fainali za mwakani za kombe la mataifa ya Afrika nchini Cameroon.
Mauritania ni moja kati ya nchi 13 ambazo zimekwisha fuzu katika kinyang'anyiro hicho kitakachozikutaninisha timu 24. Timu nane kati ya hizo zimefuzu mwishoni mwa juma hili, zikiongozwa na mabingwa wa zamani Nigeria, Ivory Coast, Morocco na Algeria.
Ivory Coast , mabingwa wa Afrika mwaka 2015, walihakikisha nafasi yao ya kufuzu walipotoka sare ya bao 1-1 na Guinea jana na matokeo hayo yakawapa nafasi wote ya kufuzu. Morocco ilijihakikishia nafasi ya kufuzu baada ya Malawi kwa mshangao kupoteza mchezo wake dhidi ya Comoro kwa mabao 2-1.
Libya ina nafasi ya kufuzu na inakabiliana na Afrika kusini mwezi Machi na kujiunga na Nigeria katika kundi lao kucheza katika fainali. hata hivyo Libya inahitaji kushinda wakati Afrika kusini inahitaji sare.
Burundi inahitaji pia sare nyumbani dhidi ya Gabon , wakati Lesotho pia nayo inaweza kufuzu iwapo itaishinda Cape Verde na Tanzania kushindwa na Uganda , baada ya jana Tanzania kuangukia pua kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Lesotho.
Mwandishi: Sekione Kitojo / dpae / ape / afpe / rtre
Mhariri: Yusuf , Saumu