Matumizi ya tumbaku katika mataifa ya bara Asia
Matumizi ya tumbaku yamekithiri katika mataifa mengi ya bara Asia. Haya ni baadhi ya mataifa ya bara hilo yalio na viwango vya juu vya matumizi ya tumbaku kulingana na shirika la WHO.
Timor Leste
Kulingana na Atlas ya tumbaku za mwaka 2015, asilimia 39.8 ya wanaume nchini Timor Leste na takriban asilimia 12.4 ya wanawake nchini humo huvuta sigara kila siku. Kila mwaka, zaidi ya raia wake 700 hufariki kutokana na magonjwa yanayohusiana na matumizi ya tumbaku.
Indonesia
Takriban asilimia 39.8 ya watu nchini humo hutumia tumbaku. Hii inaashiria idadi ya takriban watu milioni 57. Indonesia haina marufuku ya uvutaji wa sigara katika maeneo mengi ya umma. Wavutaji wengi huvuta Kretek, sigara ya kitamaduni ambayo ni mchanganyiko wa tumbaku na karafuu.
Laos
Kulingana na mratibu wa muungano wa udhibiti wa tumbaku (ASEAN) Lao, wavutaji sigara wa umri wa zaidi ya miaka 15 huchangia zaidi ya asilimia 57 ya idadi kamili ya watu. Shirika la WHO linasema tumbaku husababisha takriban asilimia 50 ya vifo vya watumiaji wake.
Mongolia
Kulingana na Atlas ya tumbaku, Mongolia imepata ufanisi katika udhibiti wa tumbaku katika miaka ya hivi karibuni. Hata hivyo, watu wanaendelea kufariki ama kuwa wagonjwa. Takriban asilimia 40.7 ya wanaume na asilimia 41 ya wavutaji wa umri wa zaidi ya miaka 15 hutumia tumbaku kila siku.
China
China ni taifa lenye idadi kubwa ya watumiaji wa tumbaku. Asilimia 44.8 ya wanaume nchini China, na asilimia 2 ya wanawake wa umri wa zaidi ya miaka 15 hutumia tumbaku kila siku. Mwaka 2016, vifo vilivyosababishwa na matumizi ya tumbaku vilifikia asilimia 24.89 kulingana na Atlas ya tumbaku .
Philippines
Kulingana na shirika la WHO, waraibu wa uvutaji sigara kati ya watu wa umri wa miaka 15 na zaidi ni asilimia 24.3. Zaidi ya watoto elfu 94 hutumia tumbaku kila mwaka. Kila mwaka, zaidi ya watu 117,700 hufariki kutokana na magonjwa yanayohusiana na matumizi ya tumbaku, kulingana na Atlas ya tumbaku ya mwaka 2015.
Nepal
Umri wa waraibu wa uvutaji tumbaku kwa watu wa miaka 15 na zaidi ni asilimia 23.7 kulingana na shirika la WHO. Kulingana na Atlas ya tumbaku, asilimia 15.68 ya vifo mnamo mwaka 2016 vilisababishwa na matumizi ya tumbaku.
South Korea
Serikali ya Korea Kusini imechukuwa hatua za kupunguza kiwango cha uvutaji wa siagara wa wanaume kwa takriban asilimia 29 ifikapo mwaka 2020 kwa kulifanya taifa hilo mahala pagumu zaidi pa kuvuta sigara. Kulingana na shirika la WHO, umri wa waraibu wa uvutaji tumbaku miongoni mwa watu wa umri wa miaka 15 na zaidi ulikuwa asilimia 23.6 mwaka 2016.
Vietnam
Uvutaji sigara ni jambo la kawaida kama katika mataifa mengine ya Mashariki Kusini mwa Asia. Mwaka 2016, ilikadiriwa kuwa asilimia 50 ya wanaume na asilimia 5 ya wanawake wanatumia tumbaku. Kituo cha elimu ya afya na mawasiliano cha Vietnam kinakadiria kuwa watu elfu 40 hufariki kila mwaka kutokana na uvutaji wa sigara.
Sri Lanka
Kulingana na shirika la WHO, umri wa waraibu wa uvutaji tumbaku miongoni mwa watu wa umri wa miaka 15 na zaidi ni asilimia 13.7. Kila mwaka , zaidi ya watu 12 300 ya watu wake wanafariki kutokana na magonjwa yanayohusiana na matumizi ya tumbaku , kulingana na Atlas ya tumbaku ya mwaka 2015.