Samani za kale ni moja wapo ya njia zinazotumika kudumisha utamaduni wa watu wa kisiwa cha Unguja, Zanzibar. Kwa baadhi matumizi ya samani hizo ni utambulisho wao wa kitamaduni na ni kitu kinachowapa fahari. Na kwa baadhi, ni bishara inayowasaidia kuendesha maisha yao. Zaidi ungana na Mohammed Khelef.