1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Matumizi ya kijeshi yaongezeka duniani

26 Aprili 2021

Pamoja na uwepo wa janga la virusi vya corona, lakini jumla ya matumizi ya zana za kijeshi duniani kwa mwaka uliopita yameongezeka kwa karibu dola trilioni 2.

https://p.dw.com/p/3sZ0a
Flugzeugträger Theodore Roosevelt | U.S. F-18 Kampfjet
Picha: Jim Gomez/AP Photo/picture alliance

Hayo yamo katima takwimu mpya zilizotolewa na Taasisi ya Kimataifa inayohusika na utafiti wa masuala ya amani, SIPRI yenye maskani yake mjini Stockholm, nchini Sweden. Taarifa hiyo inasema kumekuwepo na jumla ya matumizi ya kiasi cha dola bilioni 1,981, na kufanya ongezeko la asilimia 2.6 ikilinganishwa na mwaka 2019.

Mataifa ambayo yanaongoza katika matumzi makubwa ni Marekani, China, India, Urusi na Uingereza. Yote kwa pamoja hayo yanafanya jumla ya asilimia 62 ya jumla ya matumizi ya silaha duniani. Lakini kwa namna ya kipekee kiwango hicho kwa China kimekuwa kikiomngezeka kwa takribani mwaka wa 26 kwa mfululizo.

Janga la virusi vya corona halijapunguza matumizi ya kijeshi.

US-Panzer Symbolbild Waffenhandel
Kifaru cha jeshi la Marekani nchini RomaniaPicha: Andreea Alexandru/AP/dpa/picture alliance

Mtafiti wa SIPRI, anaehusika na Silaha na Programu ya Matumizi ya Kijeshi, Diego Lopes da Silva amesema janga la virusi la corona halukuwa na athari zozote katika matumzi ya zana za kijeshi kwa mwaka 2020. Hata hivyo aliongeza kwa sasa bado wapo katika tathimi ya endapo mataifa yataendelea katika kiwango hicho cha matumizi ya kijeshi katika kipindi hiki kingine chote cha janga la virusi vya corona.

Lakini pamoja na ongezeko hilo la fedha katika sekta ya ulinzi kwa mataifa mbalimbali lakini baadhi ya mataifa kwa kiwango kikubwa pia yalibadilisha fedha za bajeti zake kwa mpango huo na kuzielekeza katika jitihada za kukabiliana na janga la virusi vya corona. Mfano wa mataifa yalichukua mkondo huo ni pamoja na  Chile, Korea Kusini, mengine Brazil na Urusi. SIPRIinasema mataifa hayo yalitumia kiwango cha chini kuliko kili kilichoanishwa awali kwa bajeti ya 2020.

Marekani ambayo inatajwa kuwa kinara wa kutumia fedha nyingi katika sekta yake ya ulinzi, kwa mujibu wa SIPRI kwa mwaka 2020, matumizi yake ya kijeshi yanakadiriwa kufikia dola bilioni 778 likiwa ni ongezeko la asilimia 4.4 ikilinganishwa na mwaka 2019.

Kwa hatua hiyo Marekani inahesabiwa kutumia asilimia 39, ya jumla ya asilima zote za matumizi ya kijeshi duniani. Hili pia ni ongezeko la mara ya tatu mfululizo, baada ya miaka mengine saba ya jitihada za kupunguza matumizi hayo.

Chanzo: DPA