1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Matokeo ya uchaguzi wa Iraq hadi sasa

17 Machi 2010

Al -Maliki na Allawi wako bega kwa bega

https://p.dw.com/p/MUsI
Nouri al-Maliki akipiga kura.Picha: AP

Taarifa kutoka Baghdad, zinasema waziri-mkuu Nuri al-Maliki na mpinzani wake mkubwa katika uchaguzi wa Bunge la Iraq wa hivi majuzi, Iyad Allawi , wako bega kwa bega kwa muujibu wa matokeo ya hivi punde.Kila upande una viti 87 ingawa kwa jumla, waziri mkuu wa zamani Allawi, asielemea madhehebu yoyote ya kidini,anaongoza kidogo kwa kura za nchi nzima.

MATOKEO HADI SASA:

Ushirika wa waziri-mkuu Nuri Al-Maliki wa "State of Law Alliance " na ule wa Bw. Allawi wa Muungano wa wairaqi (Iraqiya Coalition) una viti 87 kila mmoja na hivyo, kura 9.000 zinatenganisha kambi hizo mbili kote nchini.Hii ni hali baada ya 79% ya kura kuhesabiwa. Lakini, kura zilizopigwa na wairaqi nje ya nchi na wakati wa upigaji kura maalumu uliotangulia kwa vikosi vya ulinzi na polisi,wagonjwa na wafungwa bado hazikuhesabiwa na Tume ya Uchaguzi ya Iraq na huenda yakashawishi mno mkondo wa matokeo ya mwisho ya uchaguzi.

Uchaguzi wa majuzi, wapili nchini Iraq tangu kupinduliwa Rais Saddam Hussein, 2003,umefanyika si zaidi ya miezi 6 kabla Marekani, kuanza kuondoa majeshi yake yanayopigana kutoka Iraq.

Wakati muungano wa waziri-mkuu wa zamani Iyad Allawi, unaongoza kidogo katika kura jumla kote nchini, Ushirika wa dola linalofuata sheria wa waziri mkuu Al-Maliki unaonmgoza kwa kura katika mji mkuu Baghdad,jimbo kubwa nchini Iraq lenye viti vingi mara 2 zaidi kuliko mkoa wowote ule wa Iraq na pia , unaongoza katika mkoa wa kusini na tajiri kwa mafuta wa Basra na watatu kwa ukubwa nchini .

KUNDI LA AL-MALIKI:

Ushirika wa waziri-mkuu Al-Maliki, halkadhalika, unaongoza pia katika mikoa mingine 5 inayokaliwa na waumini wa madhehebu ya shiia, lakini umeshindwa kuibuka usoni katika mikoa mikuu 3 isipokuwa 1tu wenye wingi wa waumini wa madhehebu ya sunni.

Muungano wa Iraqiya wa Bw. Allawi , unaongoza katika mikoa 4 miongoni mwayo, mkoa wapili kwa ukubwa wa Nineveh.Pia muungano wa Bw.Allawi , uko bega kwa bega katika kinyan'ganyiro cha mkoa 5 wa kirkuk ambako unaongoza mbele ya kundi la wakurdi kwa kura 6 tu.

KUNDI LA WASHIA:

Ushirika wa kitaifa wa Iraq (Iraqi National Alliance)- muungano unaoongozwa na vikundi vya kidini vya washiia, unaelekea kutokea 3 katika uchaguzi huu wa bunge ukiwa na viti 67 wakati kundi la wakurdi (Kurdistania), yamkini likaondokea na viti 38 tu.Hakuna kikundi kingine kinachoweza kunyakua zaidi ya viti 10 kwa jicho la matokeo yalivyo hadi sasa.Viti 15 kati ya viti jumla 325 vya Bunge la Iraq, vimewekwa kando kufidia vikundi visivyopata uwakilishi au jamii za wairaqi wachache na hivyo, havija jumlishwa katika hesabu hii.

UPINZANI:

Vikundi vya Upinzani, vimelalamika kuwa mizengwe imepitishwa katika uchaguzi huu.Maafisa wa usalama wameelezea swasi wasi kuwa kipindi kirefu kitakacho fuatia matokeo ya uchaguzi huu cha kuundwa serikali ya muungano, chaweza kuvipa vikundi vya waasi na kile cha Al Qaeda, fursa ya kuendelea kuichafua Iraq isipate utulivu.

Mwandishi: Ramadhan Ali/ AFPE

Uhariri: Abdul-Rahman