Matokeo ya uchaguzi nchini Ethiopia
22 Juni 2010Hakuna kitakachokua kama zamani baada ya ushindi wa asili mia 99.6 wa chama tawala nchini Ethiopia.Washirika wa Ethiopia wanabidi kuishinikiza serikali ya mjini Addis Ababa.
Asili mia 99.6 au viti 545 kati ya 547 vya bunge-hiyo mpya hiyo na nadra kushuhudiwa mahala kokote kwengine barani Afrika matokeo ya uchaguzi yakapindukia asili mia 80.Suala ambalo wachunguzi wa Ethiopia wanajiuliza siku moja baada ya matokeo ya uchaguzi kutangazwa ni "kwanini udanganyifu uwe bayana hivyo?
Waziri mkuu Meles Zenawi ataliwakilisha kwa mara nyengine tena bara la Afrika mkutano wa viongozi wa kundi la G-20 utakapofunguliwa mjini Toronto mwishoni mwa wiki.
Anakwenda huko akiwa mshirika aliyesubutu kufanya udanganyifu katika mahala yanakokutikana makao makuu ya Umoja wa Afrika-jambo ambalo hata mshirika wake Marekani amelilaani.
Baada ya balaa la uchaguzi wa mwaka 2005,pale ushindi ulipogharimu maisha ya waandamanaji 200,safari hii serikali inaonyesha kupindukia mipaka.Makada mikoani wanaonyesha kupewa amri ya kutozubaa.
Kwa kujitangazia ushindi wa asili mia 99.6 za kura,serikali imebainisha moja kwa moja imegeuka "kuwa utawala unaoendelea wa kimla"-neno kiimla" ndo la kushadidiwa hapo.Washirika mijini Washington,Brussels na Berlin watalazimika kukabiliana na hali hiyo."Hali haistahiki tena kuwa kama zamani"-la sivyo, viongozi na hasa rais wa Marekani atapoteza imani ya waafrika hata kabla ya kufafanua siasa ya nchi yake kuelekea bara la Afrika."Maendeleo yanategemea utawala bora na wanaobeba dhamana ni waafrika wenyewe" alisema hayo rais Barack Obama alipokua ziarani nchini Ghana.
Ethiopia,mshirika wa Washington katika kupambana na magaidi katika pembe ya Afrika imegeuka mzigo na sio tuu kwa Marekani bali pia kwa Ujerumani inayoifadhili vyema Ethiopia.Wananchi wa Ethiopia wanachukizwa tangu zamani na kile kinachofanywa na wale wanaotajikana kama "washirika wa maendeleo kutoka nchi za magharibi."
Kwasababu wanahisi washirika hao wanaona bora watangulize mbele shati yaani mapambano dhidi ya magaidi katika pembe ya Afrika na mali ghafi badala ya suruwali yaani mfumo wa kidemokrasi na haki za binaadam.Matokeo yake ni kwamba vijana wa Ethiopia wanaziangalia Ulaya na Marekani kupitia Beyoncé na Manchester United na sio kama mfano mwema wa kuigizwa wa mfumo wa kidemokrasi.
Kimoja cha maana lakini kimepatikana:nacho ni kwamba upande wa upinzani ambao hapo awali ulikuwa umegawanyika na kuingia katika uchaguzi bila ya mpango maalum,hivi sasa hauna budi isipokua kujiimarisha.Inamaanisha viongozi wepya na fikra mpya ili kuweza kuendeleza mapambano ya kinadharia ya kimambo leo na zaidi ya hayo kuweza kuwavutia zaidi vijana.
Mwandishi:Schadomsky,Ludger/
Hamidou Oummilkheir
Imepitiwa na:M.Abdul-Rahman