1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mateka watatu nchini Colombia kuachiliwa karibuni

27 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/Cgtl

CARACAS.Rais Hugo Chavez wa Venezuela amesema kuwa mateka watatu wanaoshikiliwa na waasi wa Colombia wenye msimamo wa kimax, wataachiwa hivi karibuni.

Rais Chavez amekuwa mpatanishi katika mzozo wa Colombia na waasi wa jeshi la kimapinduzi la Colombia FARS ambao wamekuwa wakiwashikilia mateka hao toka mwaka 2002.

Mateka hao ni aliyekuwa mgombea urais wa Colombia bi Ingrid Bentacourt pamoja na meneja wake wa kampeni Clara Rojas.

Mume wa bi Ingrid, Juan Carlos le Compte alielezea furaha yake baada ya Rais Chavez kutoa taarifa hiyo.