Matayarisho ya kuwarejesha nyumbani mateka watatu kutoka kwa waasi wa Colombia yakamilika
28 Desemba 2007Matangazo
CARACAS:
Venezuela inajitayarisha kuanzisha mpago wa kutuma ndege za kuwachukua mateka watatu wanaoshikiliwa na waasi wa Colombia.
Wajumbe wa kigeni watajiunga na msfara huo.Miongoni mwa hao ni rais wa zamani wa Argentina Nestor Kircher. Mmoja wa mateka- aliekuwa kigombea kiti cha makamu wa rais wa colombia-Clara Rojas alichukuliwa mateka na wasi hao wakimaxisti miaka 6 iliopita na kuwekwa katika kambi za siri katika msitu wa nchi hiyo.Rais wa Venezuela-Hugo Chavez amesema kubidhiwa rasmi kwa mateka hao kunaweza kufanyika Ijumaa.Colombia imetoa kibali kwa ndege tatu pamoja na helkopta mbili za Venezuela kuwachukua wanawake wawili pamoja na mtoto mmoja kutoka maeneo walikokuwa wanashikiliwa mateka.