Matarajio ya Wakenya baada ya ziara ya Koffi Annan nchini humo
9 Oktoba 2009Matangazo
Mashirika yasiyo ya kiserikali yanasema linalohitajika ni
Annan kubuni jopo la uchunguzi litakaloyashirikisha mashirika ya
kiraia na viongozi wa dini, ili wawasukume viongozi wawajibike
kuharakisha hatua za mageuzi, la sivyo ziara za Annan zitakuwa ni za
bure. Munira Muhammad alizungumza na Cyprian Nyamwamu, mkurugenzi wa shirika la
National Convention Executive Council, mwavuli wa asasi za kiraia
nchini Kenya. Alianza kwa kumuuliza Iwapo viongozi wa kisiasa
nchini Kenya wanamheshimu Annan, Wakenya watarajie nini kutoka
kwa Rais Kibaki na Waziri mkuu Raila Odinga.
Mwandishi: Munira Muhammad.
Mhariri:Hamidou Oummilkheir