Eneo la Turkana nchini Kenya, ni mojawapo ya maeneo maskini zaidi nchini humo, likikabiliwa na hali ya joto, na umaskini wa kutupa. Lakini tumaini limeanza kuchomoza kwa wakaazi wa eneo hilo kufuatia ugunduzi wa mafuta. Katika makala hii ya Mtu na Mazingira, Shisia Wassilwa anaagazia matumaini, wasiwasi na athari za kimazingira vinavyoambatana na ugunduzi huo.