Tuliyo nayo mchana huu: Kiongozi wa muda mrefu nchini Gambia, Yahya Jammeh amebadili kauli na kukataa kushindwa uchaguzi. Rais wa Marekani Barack Obama ameagiza ripoti ya uchunguzi juu ya udukuzi huku kukiwa na wasiwasi wa kuingiliwa na mataifa ya nje katika uchaguzi wa rais wa mwaka huu. Rais wa Ghana John Mahama amekubali kushindwa katika matokeo ya uchaguzi mkuu uliofanyika Jumatano wiki hii.