1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUfaransa

Matamshi ya balozi wa China yazua taharuki

23 Aprili 2023

Matamshi yaliyotolewa na balozi wa China nchini Ufaransa akihoji uhuru wa mataifa yaliyojiengua kwenye muungano wa Kisovieti, yameibua ghadhabu miongoni mwa mataifa hayo na Ufaransa.

https://p.dw.com/p/4QSUj
bendera za Umoja wa Ulaya nje ya jengo la umoja huo mjini Brussels
Mengi ya mataifa yaliyojiengua kwenye muungano wa Kisovieti ni wanachama wa Umoja wa UlayaPicha: Kenzo Tribouillard/AFP/Getty Images

Matamshi hayo yameibua mashaka sio tu nchini Ukraine, lakini pia kwa jamhuri zote zilizojiengua na kuwa mataifa huru baada ya kuanguka kwa Muungano wa Kisovieti mwaka 1991, ambapo mengi yao ni wanachama wa Umoja wa Ulaya.

Taarifa iliyochapishwa usiku wa jana na wizara ya mambo ya nje ya Ufaransa imesema imefadhaishwa na matamshi hayo ya Balozi Lu Shayne na kuongeza kuwa, ni juu ya China kusema iwapo matamshi kama hayo yanaakisi nafasi yake.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Latvia Edgars Rinkevics amesema matamshi yanayohoji sheria ya kimataifa na uhuru wa mataifa hayakubaliki kabisa, na kuongeza kuwa wanasubiri ufafanuzi wa China na kuibatilisha kauli hiyo. 

Soma Zaidi: Von der Leyen awarai viongozi wa Ulaya kushikamana kuikabili China