1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mataifa kadhaa yakutana kutafuta amani ya Somalia

31 Mei 2012

Wakati Somalia kwa miongo miwili sasa ikiwa katika vita vya wenyewe kwa wenyewe wawakilishi wa mataifa zaidi ya 54 wanakutana huko Istanbul-Uturuki kujadili mustakbali wa taifa hilo la Mashariki mwa Afrika.

https://p.dw.com/p/155KC
Wanajeshi kutoka mataifa mengine ya Afrika
Wanajeshi kutoka mataifa mengine ya AfrikaPicha: picture-alliance/ dpa

Huku Majeshi Umoja wa Afrika yakiijongelea ngome iliyosalia ya wanamgambo wa Al-Shabab.

Taifa hilo lililokosa serikali imara kwa miongo miwili sasa linatafutiwa mustakbali mpya katika mkutano huo ulio ambapo unatarajiwa kulizingatia suala la misaada kwa nchi hiyo. Miongoni mwa washiriki wakuu ni pamoja na Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-Moon.

Akifungua mkutano huo Naibu Waziri Mkuu wa Uturuki Bekir Bozdag amesema baada ya hali ya matatizo nchini Somalia kwa muda mrefu katika vita na migogoro isiyokwisha, sasa ni wasaa wa amani na usalama. Somalia inawakilishwa na Rais Sharif Sheikh Ahmed katika mkutano huu.

Wasomali wakiwa ukimbizini
Wasomali wakiwa ukimbiziniPicha: dapd

Mkutano huu unafanyika baada ya mkutano wa London mwezi Februari mapema mwaka huu. Mambo kadhaa yalijadiliwa na maafisa wa ngazi za juu na wafanyabiashara kadhaa.

Wakati mkutano huo ukiendelea vikosi vya Umoja wa Afrika vimeingia mji wa Afwadow ambao ni ngome iliyosalia ya wamgambo wa Al Shabab .

Mji wa Afmadow ulikuwa unalengwa kwa muda mrefu na vikosi vya Kenya tangu vilipolivamia eneo la Kusini mwa Somalia Oktoba mwaka jana kabla ya majeshi hayo ya Umoja wa Afrika kujiunga nao. Akizungumza hali hiyo msemaji wa Jeshi la Kenya Colonel Cyrus Oguna amesema bado mapigano yanaendelea lakini ana imani watashinda.

Wanajeshi wa Umoja wa Ulaya wanaopambana na maharamia
Wanajeshi wa Umoja wa Ulaya wanaopambana na maharamiaPicha: picture-alliance/dpa

Wanamgambo hao wa Al Shabab waliojikita katika mji huo waliwarudisha nyuma wanajeshi wa Kenya na Vikosi vya Umoja wa Afrika miezi iliyopita na kuwazuia kupenya kufika Kismayo. Mji wa Afmadow upo umbali wa Kilometa120 ndani ya Somalia kutoka mpaka wa Kenya.

Kikundi hicho kikiwa bado kinalidhibiti eneo kubwa la kusini mwa Somalia kuna dalili ya wanamgambo hao kuondoka kwani wameonekana wakitoroka kupitia bandari ya Kismayo. Nayo Majeshi ya Umoja wa Afrika yenye jumla ya askari 11,000 yameweka wazi kuwa operesheni hiyo itakamilika katika kipindi cha miezi mitatu kuanzia sasa.

Mwandishi:Adeladius Makwega/AFPE

Mhariri : Mohammed Abdul-Rahman