Mataa ya Krismasi katika barabara za Ulaya
Huku sherehe zikiwa zinanukia, ni wakati wa mapambo na mataa ya kumetameta. Bustani na barabara za Ulaya zinang'aa kwa mataa. Furaha ya Krismasi iko nasi kwa wakati mwengine.
Kurfürstendamm mjini Berlin
Umbo kubwa la Santa Claus lililowashwa mataa na rafiki zake liko katika eneo la Ku'damm, kama wenyeji wanavyopenda kuliita. Wakaazi wa Berlin mwaka huu wamejitahidi kuipamba bustani yao. Kuna miti 650 na mataa yamewekwa umbali wa kilomita 230.
Paris' Champs-Élysees
Mataa yanametameta katika miti ya Champs-Elysees mjini Paris, bustani inayosemekana kuwa maarufu zaidi Ulaya. Mataa hayo ya kumetameta yaliyowekwa na kampuni ya Blachere illuminations, kwa mara nyengine yataing'arisha barabara ya Avenue des Champs-Elysees mwaka huu hadi Januari 8 2018.
Barabara ya London Oxford
Barabara maarufu zaidi London imepambwa kwa mataa ya theluji 1778. Mapambo hayo yanayoitwa "mataa ya Krismasi" yamefanyika katika barabara hiyo tangu 1959. Huku barabara hiyo ikiwa na watalii zaidi ya 500,000 kwa siku, barabara hiyo ya Oxford inaorodheshwa miongoni mwa barabara zenye shughuli chungunzima za ununuzi barani Ulaya.
Graben mjini Vienna
Mji Mkuu wa Austria unameta meta kwa mataa ya ajabu. The Graben ni eneo la watu kutembea kwa miguu katikati mwa Vienna huku majengo ya karne ya 17 na 18 yakimetameta katika mapambo ya Krismasi. Maduka ya kihistoria na kitamaduni ya kahawa mjini Vienna yanapatikana hapa.
Bustani ya Anspach Brussels
Bustani ya Anspach katika Mji Mkuu wa Ubelgiji una wageni tele wote wakiwa wanazuru maonesho ya Krismasi. Sehemu ya bustani hiyo iliyojaa wageni iliwekwa kama eneo la watembea kwa miguu mwezi Juni mwaka 2015.
Calle Velazquez mjini Madrid
Eneo la kati la Mji Mkuu wa Uhispania limepambwa wakati wa Krismasi. Wabunifu na wasanifu majengo maarufu ndio waliohusishwa katika kuzipamba barabara na viwanja tofauti kwa njia ya ubunifu na kuvipatia hali ya msimu wa Krismasi.
La Rambla mjini Barcelona
Mji wa bandari wa Uhispania Barcelona, unaleta uhai wa msimu wa Krismasi kwa maelfu ya mataa yanayowaka na kumetameta katika eneo la La Rambla. Eeneo hilo la kutembea lililoko karibu na bahari lina urefu wa karibu kilomita 1.3 na ni kivutio cha watalii kutoka kote duniani. Vibanda vingi, maduka ya kuuza kumbukumbu, wasanii wa barabarani, wanamziki na wauza maua wanaipatia barabara hiyo uhai wake.
Barabara ya Bahnoff mjini Zurich
Na anga yake ya samawati, Lucy amerudi katika mji wa Uswisi wa Zurich. Jina lake limetokana na hafla ya kuwashwa mataa ya Krismasi ambayo imekuwa ikifanyika katika barabara hiyo ya Bahnoff tangu mwaka 2010. barabara hiyo ni maarufu kote duniani kwa maduka yake yenye bidhaa za bei ghali na bei ya kukodi maduka katika barabara hiyo ndiyo bei ya juu zaidi Ulaya.
Via Condotti mjini Roma
Barabara nyengine maarufu sana inayopendwa katika masuala ya ununuzi - Via Condotti. Barabara hii ikiwa imezungukwa na jengo na kihistoria la Palazzi, inajumuisha idadi kubwa ya maduka ya mitindo. Kila mwaka msimu wa Krismasi, mataa ya kumetameta yanaleta uhai katika shughuli chungunzima zilizoko katika barabara hiyo.
Njia ya Kifalme ya Warsaw
Kutoka wiki ya kwanza ya Desemba, njia ya kifalme ya Warsaw inakuwa njia ya kupendeza ya Krismasi. Inaanzia katika Kasri, njia hiyo ina urefu wa kilomita kumi, jambo linaloifanya kuwa mojawapo ya njia ndefu zaidi kivyake duniani. Bustani, makasri ya zamani na majumba makubwa yanaizunguka barabara hii katika Mji Mkuu wa Poland.