1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Masoko ya hisa yashuka baada ya Trump kutangazwa mshindi

9 Novemba 2016

Masoko ya hisa yameshuka kwa kasi leo jumatano, dola imeshuka zaidi ilikinganishwa na euro pamoja na yeni baada ya Donald Trump kutangazwa kuwa mshindi wa urais Marekani, wafanyabiashara na wachumi wamekata tamaa.

https://p.dw.com/p/2SPIb
US-Präsidentschaftswahl 2016 - Sieg & Rede Donald Trump
Picha: Getty Images/S. Platt

Masoko ya fedha yametetereka ghafla kufuatia ushindi wa Donald Trump hasa ikizingatiwa kuwa katika kampeni zake amekuwa akitumia maneno makali akizungumzia nia ya kutaka kuvunja baadhi ya mikataba ya kibiashara na kuanzisha sheria kali za kudhibiti wahamiaji. Katika kampeni zake pia Trump alitishia kuwafunga wapinzani wake wa kisiasa.

Msimamo wa Trump wa utatanishi dhidi ya China pamoja na washirika wengine wa kibiashara, umebadili mitazamo muhimu kutokana na kutokuwepo kwa mipango yenye maelezo elekevu, jambo ambalo limewaacha wengi katika hofu na wasiwasi juu ya maamuzi ya Trump mara atakapoingia Ikulu.

Sarafu ya Mexico peso, imeanguka kupita kiwango wakati ambapo raslimali zisizotikiswa thamani yake zikipanda bei , ambapo dhahabu imepanda kwa zaidi ya asilimia tano. Dhamana za Ujerumani zimeongezeka thamani. Serikali za Japan na  Korea kusini zimepanga kufanya mazungumzo ya haraka kutokana na wasiwasi na hofu ya kujitokeza athari katika soko la biashara ya hisa.

Matumaini ya wengi yatoweka

Matumaini ya awali ambayo yalikuwepo kwa kutarajia Ushindi kwa HillarY Clinton yalitoweka  hasa baada ya kuonekana kwamba Donald Trump amepata ushindi wa kura nyingi zilizohitajika kutimiza ndoto yake ya kuingilia Ikulu ya White House. Masoko yamekumbwa na mtikisiko kwa sababu wawekezaji wengi walitarajia ushindi wa Clinton ambaye walimuona kama chaguo salama akilinganishwa na Trump ambaye anaonekana hatokuwa na sera madhubuti. Wengi wanahofia kuwa sera za Trump zinaweza kuiagusha Marekani taifa ambalo linaongoza kiuchumi duniani.

USA 20 Dollar Schein Präsident Jackson
Dola ya MarekaniPicha: picture alliance/dpa/D. Kalker

Sarafu za nchi mbalimbali zimedondoka thamani yake kabla ya shughuli za kibiashara kumalizika, ambapo Yeni ya Japan imeanguka kwa asilimia 5.4 wakati masoko ya hisa nayo ya HongKong yakianguka kwa asimilia 2.2 na Shangai kwa silimia 0.6.

Katika biashara ya soko la hisa mapema leo mjini London, bara Ulaya limekabiliwa pia na kudondoka kwa thamani ya sarafu zake kwa kiwango cha ssilimia 1.9, soko la hisa la mjini Paris limedondoka kwa asilimia 2.8 na huko mjini Frankfurt nchini Ujerumani vilevile soko la hisa limepata mfadhaiko na kuporomoka kwa asilimia 2.9

Katika hali hiyo ya mfadhaiko wa masoko duniani kote waziri wa fedha wa Mexico  Jose Antonio Maede na gavana wa benki kuu Augustin Carsterns watazungumza na waandishi wa habari baadae leo kuelezea mikakati baada ya kushuka kwa thamani ya sarafu ya peso.

Mwandishi: Celina Mwakabwale/ AFP/AP

Mhariri:Yusuf Saumu