Masoko ya fedha : Dollar ya Marekani yapaa dhidi ya Euro.
25 Oktoba 2008Mzozo mkubwa wa kifedha duniani umesababisha wawekezaji duniani kote kuacha kutumia sarafu za nchi zao na kutafuta hifadhi katika sarafu ya dola ya Marekani , mtindo ambao wadadisi wengi wanauona kuwa utaendelea kwa muda mrefu.
Dollar imepanda thamani kwa karibu asilimia 12 dhidi ya sarafu ya Euro tangu kuanza mwaka huu. Imeendelea kupanda kwa kiwango cha juu kabisa mwezi huu dhidi ya sarafu ya Euro tangu kuanzishwa kwake 1999.
Sarafu ya dollar pia imepanda dhidi ya sarafu zenye mafanikio makubwa kama dola ya Australia na New Zealand, ikipanda kwa kaisi cha asilimia 25. Imeadhibu pia sarafu za nchi zinazoitwa za masoko yanayoinukia , ambayo yamekuwa kipenzi cha wawekezaji kutokana na mapato yao makubwa ya fedha za kigeni na utoaji wa riba zenye ushindani.
Baadhi ya wachunguzi wanasema kuwa si kutokana na Marekani na dolla yao kuwa ndio sababu ya kimbilio hilo. Kwani tangu hapo , kimbunga hicho kilianzia huko, kuanzia pale mabenki yalipoporomoka kutokana na mikopo ya nyumba isiyolipika ambayo iliibuka majira ya joto mwaka 2007 wakati bei za nyumba zilipoporomoka.
Muhanga imekuwa ni duniani nzima. Wawekezaji wametumia fedha za kukopa kuongeza mapato yao katika miaka ya hivi karibuni. Mikopo hii sasa inahitajiwa na wakopeshaji na iwapo deni lilithaminiwa katika sarafu ya dollar , ambapo ukweli ni kwamba , mengi ya madeni hayo yamethaminiwa hivyo, matokeo ni kwamba kunakuwa na mbinyo kiasi, ni lazima kupiga mbio kutafuta dollar ili kulipa mikopo hiyo.
Hekaheka za mabadilishano ya fedha za kigeni, zinaonyesha mabadiliko makubwa ya msimamo na haja ya kuzuwia hasara katika mali nyingine zilizothaminiwa katika dollar, amesema Avery Shenfeld, mchumi mwandamizi katika CICB World Markets mjini Toronto.
Dollar inaweza kupata thamani ya juu zaidi kinyume na thamani yake ya kweli, katika wakati huu wa msukosuko na hakuna kinachoweza kuzuwia dollar ya Marekani kufikia kiwango cha dola 1.20 dhidi ya Euro, ameongeza.
Hata hivyo ishara za kitaalamu zinaonesha kuwa kasi ya dollar ya Marekani kupanda thamani huenda ikalazimika kupungua hivi karibuni kutokana na , ni umbali gani imeweza kupanda katika muda wa miezi mitatu iliyopita. Kwa mujibu wa takwimu, sarafu ya Euro imeuzwa mno katika muda mfupi na mrefu. Kiufundi dola ambayo imenunuliwa kupita kiasi inaelekea katika eneo la kununuliwa zaidi. Huu hata hivyo wanaonya wachunguzi wa mambo kuwa ni mchezo hatari kwa wakati huu kwa muuzaji ambaye anategemea tu kipimo cha hali ya kuyumba huku na huko kwa sarafu, kwa hiyo inabidi kuwa makini na kuzuwia kabisa uuzaji ama ununuzi, anasema Jack Crooks, rais wa shirika la ushauri wa uwekezaji katika sarafu la Black Swan Capital mjini Palm City katika jimbo la Florida nchini Marekani.
Mmoja kati ya utabiri mkubwa kuhusu Euro umetolewa na benki ya BNP Paribas, ambayo imetabiri kuwa Euro itashuka hadi dollar 1.13 ifikapo robo ya kwanza ya mwaka 2010. Wiki iliyopita iliuzwa kwa dola 1.28.
Euro imeshuka kwa zaidi ya asilimia 20 dhidi ya Dollar tangu sarafu hiyo kufikia kiwango cha juu kabisa cha dola 1.60 katikati ya Julai mwaka huu.
Na ni rahisi kujua ni kwasababu gani. Katika mwezi mmoja uliopita, benki kadha za Ulaya zililazimika kuokolewa, ukiwa ni msisitizo wa hali ya mzozo wa madeni duniani. Wachumi pia wanaamini kuwa juhudu kubwa zilizochukuliwa na benki kuu na serikali kusaidia mfumo wa fedha wa dunia , ikiwa ni pamoja na baadhi ya taasisi kubwa za kifedha za Ulaya , hazitatosha kuzuwia eneo la mataifa yanayotumia sarafu ya Euro kutumbukia katika kudorora kwa uchumi.
►◄