1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mashirika ya UN yaomba dola bilioni 5.6 kuwasidia Waukraine

15 Februari 2023

Mashirika mawili ya Umoja wa Mataifa yametoa ombi la kuchangisha dola bilioni 5.6 za kuwasaidia Waukraine walioathirika zaidi na uvamizi wa Urusi.

https://p.dw.com/p/4NWDh
USA UN-Sonderbeauftragter Martin Griffiths
Picha: Xie E/Xinhua News Agency/picture alliance

Tangazo hilo, lililotolewa kwa pamoja na Ofisi ya Umoja wa Taifa ya Uratibu wa Maswala ya Kiutu - OCHA na Shirika la Kuwashughulikia Wakimbizi la UNHCR imejiri siku chache kabla ya kumbukumbu ya mwaka mmoja tangu kuanza vita hivyo mnmao Februari 24. 

Umoja wa Ulaya waahidi kusimama na Ukraine bila kuchoka

Mkuu wa Ofisi ya Uratibu wa misaada ya Kiutu wa Umoja wa Mataifa Martin Griffiths ameziomba serikali, watu, na mashirika ya kijamii kote ulimwenguni kutoa michango yao kwa ukarimu.

Mpango wa Msaada wa Kiutu kwa ajili ya Ukraine, ambao unajumuisha mamia ya mashirika ya nchini Ukraine, unahitaji ufadhili wa dola bilioni 3.9. wakati Mpango wa Msaada kwa Wakimbizi wa Ukraine ukiomba dola bilioni 1.7.