1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mashirika ya kitu yatapa kupeleka misaada Ethiopia

Josephat Charo
24 Julai 2024

Mashirika ya misaada yanahangaika kupeleka misaada inayohitajika kwa dharura katika maeneo ya kusini mwa Ethiopia ambako maporomoko ya tope yamewaua watu zaidi ya 200.

https://p.dw.com/p/4iepF
Ethiopia-Maporomoko ya ardhi
Watu zaidi ya 200 wamekufa kwenye maporomoko ya ardhi huko EthiopiaPicha: Gofa Zone Government Communication Affairs Department

Mashirika ya misaada yanahangaika kupeleka misaada inayohitajika kwa dharura katika maeneo ya kusini mwa Ethiopia ambako maporomoko ya tope yamewaua watu zaidi ya 200katika janga baya kabisa kuwahi kurekodiwa katika taifa hilo la pembe ya Afrika.

Umati wa wati walikusanyika katika eneo la janga hilo lililotokea eneo lililo mbali na la milima la jimbo la Ethiopia Kusini huku wakazi wakitumia au mikono yao kufukua tope kuwatafuta wahanga na manusura.

Kufikia sasa wanaume 148 na wanawake 81 wamethibitishwa wamekufa baada ya maporomoko hayo ya tope yaliyotokea siku ya Jumatatu katika manuspaa ya Kencho-Shacha katika ukanda wa Gofa.