Waangalizi: Hali Gaza imefikia kiwango cha kutisha
15 Februari 2024Jumuiya ya kimataifa imeongeza shinikizo la kuupinga mpango wa Israel wa kufanya kile imekitaja "operesheni kubwa" kwenye mji wa Rafah ulio kusini mwa Gaza eneo ambalo zaidi ya Wapalestina milioni 1.5 wamekwama.
Mashirika ya kibinaadamu yanaonya kuwa kuendesha operesheni za misaada katika eneo hilo huenda isiwezekane kabisa hivi karibuni.
Soma pia:CPJ: Waandishi 99 waliuawa kufuatiamzozo wa Israel-Hamas
Wakuu wa shirika la msalaba mwekundu, Madaktari wasio na Mipaka, na lile la misaada la Umoja wa Mataifa wamewaambia mabalozi mjini Geneva kuwa hali huko Gaza inafikia kiwango ambacho haitzakuwa kosa la mashirika ya kiutu kama watu watateseka, bali itakuwa ni kosa la wale watakaoamua kuruhusu hilo kutokea.
Wakati hayo yakijiri, jeshi la Israel limesemalimewakamata wanamgambo kadhaa wa Hamas, lilipoivamia hospitali kuu ya mji wa kusini mwa Gaza wa Khan Younis. Operesheni hiyo kwenye hospitali ya Nasser ilisababisha kifo cha mtu mmoja.