1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mashindano ya riadha Ulimwenguni Berlin

19 Februari 2009

Mashindano makuu ulimwenguni mwaka huu Ujerumani:

https://p.dw.com/p/GxUz
Nembo ya mashindano ya IAAF Berlin,2009Picha: DW / Boettcher

Miezi 6 kutoka sasa , wanariadha kutoka kila pembe ya dunia na hasa Kenya na Ethiopia,mataifa kuu ya riadha ulimwenguni, watawasili Berlin,kwa mashindano ya 12 ya Ubingwa wa riadha ulimwenguni-World Athletics Championship.Kuanzia August 15 hadi 23,wanariadha 1800 kutoka nchi 213 wataania medali za dhahabu,fedha na shaba katika mashindano 47 mbali mbali.

"Haya ni mashimndano makubwa kabisa ya riadha baada ya yale ya olimpik yakiushirikisha ulimwengu mzima.Ndio maana mashindano haya yana maana maalumu."

Asema Clemens Prokop,Rais wa Shirikisho la Riadha la Ujerumani na mwenyekiti wa Kamati ya Maandalio ya mashindano hayo:Anaongeza:

"Katika mipango ya maandalio tupo usoni kabisa na hata kiuchumi na kifedha kila kitu kinakwenda barabara."

Bajeti ya maandalio ya mashindano haya ubingwa wa riadha ulimwenguni-yapili kufanyika katika ardhi ya Ujerumani baada ya yale ya Stuttgart 1993,ni Euro milioni 44.Katika kima hicho Euro milioni 15 zitatokana na uuzaji wa tiketi.Hadi sasa kati ya tiketi 500.000,laki 2 zimeshauzwa.Ukilinganisha kwahivyo na mashindano mengine ya riadha ulimwenguni, ni matokeo mazuri kabisa-asema Bw.Prokop:

"Azma yetu lakini ni kufanya hata bora zaidi ili yakiingia majira ya kiangazi,tiketi zote ziwe zimeshauzwa."

Hivi sasa Kamati ya maandalio imeshajipatia wafadhili 2 kati ya 5 wa kitaifa inaotapia .Rais wa shirikisho la riadha la ujerumani anataka kupiga mafano kuitembeza Ujerumani kuwa ni kituo cha mashindano makuu ya kimataifa.Anasema jiji la Berlin kila mara lisisahauliwe inapozingatiwa kuandaa mashindano ya kilimwengu kama haya.Kwa, anasema azma ni kuutembeza uzuri wa mji huu kwani, mashindano hayo yataoneshwa kwa TV hadi nchi 190 duniani na kuonekana na wanadamu kati ya bilioni 6-8.

Kwa mara ya kwanza katika historia ya mashindano haya ya riadha ulimwenguni, mbio za marathon na mashindano ya kutembea kwa haraka ,yatabidi kupitia mjini tu.

"Tunataka kuonesha kuwa michezo ya kispoti inawaunganisha wote na kuwa kile kinachowaleta pamoja walimwengu kinaweza kuzika tofauti zinazowatenganisha."-asema Bw.Prokop.

Imepangwa kuwsa na eneo maalumu kwa mashabiki kusherehekea sawa na vile ilivyokuwa katika Kombe la dunia 2006 nchini Ujerumani.

Bw.Prokop hana shaka kabisa kuwa mashindano haya yatafanikiwa mno na kwa timuya wanariadha wa Ujerumani anatazamia lakini medali moja tu. Christina Obergfoll ndie mwanariadha wakike anaewekewa tamaa kuja na medali ya shaba .Atashiriki mashuindano haya akiwa mbele ya mashabiki wa nyumbani Berlin.

"Fursa hii ni wanariadha wachahe walionayo na hivyo , ni jambo la kufurahisha mno."

Msichana huyo mwenye umri wa miaka 27 anaazimia kufika hadi finali kwa kurusha mkuki hadi mita 70.Na hajali masafa hayo yatamfikisha wapi mwishoe katika mashindano hayao.

Wanariadha wa Afrika mashariki na hasa wale wa Kenya na Ethiopia,lakini pia kutoka Afrika ya kaskazini kama Morocco na Algeria, watapania kurudi nyumbani kutoka Berlin kama kawaida yao na medali zote kuanzia masafa ya kati ya mita 800 hadi marathon.Na hasa marathon akina Gebreselłassie wa Ethiopa na mkenya Paul Tergat wameweka rekodi za dunia si kwengineko ,bali mjini Berlin. Gebreselassie ndie kwa kweli anaetembeza biramu la mashindano haya ya 12 ya riadha ulimwenguni kabla kulia bunduki hapo August 15 mwaka huu.