1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mashindano ya kombe la kandanda la dunia la wanawake yaanza leo.

26 Juni 2011

Ufaransa yaibwaga Nigeria na Ujerumani kuchuana na Canada

https://p.dw.com/p/RVuF
Picha: dapd

Mashindano ya kombe la kandanda la dunia la wanawake 2011, yanasubiri mchuano wa pili mjini Berlin hivi punde likitarajiwa kuwa pambano la kukata na shoka kati ya wenyeji na mabingwa mara mbili wa kombe hilo -Ujerumani na Canada. Mashindano hayo kimsingi yalifunguliwa jana usiku katika hafla maalum ilioafanyika mjini Frankfurt na kutangazwa moja kwa moja kwa njia ya televisheni.

Mechi ya ufunguzi rasmi imemalizika punde ambapo waakilishi wa Afrika Nigeria walimenyana na Ufaransa na Ufaransa kuondoka na ushindi wa bao moja kwa bila lililopachikwa na Delie katika dakika ya 56, baada ya kuwa sare bila kufungana hadi mapumziko.

Ufaransa ndiyo ilioonekana kuutawala zaidi mchezo.

Ujerumani ndiyo Mabingwa watetezi baada ya kulinyakua kombe kwa mara ya pili 2007 ushindi uliofuatia ule wa awali 2003.

Itakumbukwa katika mechi ya kirafiki Septemba mwaka jana Ujerumani ambao pia ni mabingwa watetezi wa kombe la kandanda la mataifa ya Ulaya ,iliiadhibu vibaya Canada iliomaliza nafasi ya nne katika mashindano ya kombe la dunia 2003 kwa kuilaza mabao 5-0 na mwezi Novemba miwili na nusu iliopita, ikaitandika Nigeria jumla ya mabao 8-0 katika mechi nyengine iliochezwa pia katika uwanja wa nyumbani.

Brazil washindi wa pili wakati wa kombe la dunia 2007 nchini China, wamepangwa kundi moja na Australia, Norway na wawakilishi wa pili wa Afrika, Guinea ya Ikweta likiwa ni kundi D. Norway ina historia ndefu ya kombe la dunia la wanawake na ilikuwa bingwa 1997 katika fainali dhidi ya Ujerumani.

Kundi B linaonekana kuwa kundi rahisi zikiwemo Japan, Mexico, New zeland na Uingereza.

Kundi C, linaloitwa kundi la kifo kutokana na kuzikutanisha timu ngumu, lina Marekani, Korea kaskazini, Colombia na Sweden.

Ama mashabiki wa soka barani Afrika bila shaka wanazikodolea macho Nigeria mabingwa wa bara hilo na Guinea ya Ikweta.

Rais wa Shirikisho la kandanda la kimataifa FIFA Joseph Blatter amesema, mashindano hayo ya Kombe la Dunia, ni tukio muhimu la maendeleo yaliyopatikana katika kandanda linalochezwa na  

Mwandishi:Mohammed Abdul-Rahman/dpa

Mhariri: Prema Martin