1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mashambulizi ya Urusi yauwa wawili Kharkiv

Hawa Bihoga
30 Aprili 2024

Gavana wa jimbo la Kharkiv kaskazini mashariki mwa Ukraine, Oleh Synehubov , amesema mashambulizi ya Urusi yameuwa watu wawili na kujeruhi wengine sita baada ya vikosi vya Urusi kutumia 'mabomu ya kuelekezwa.'

https://p.dw.com/p/4fLVM
Ukraine Volodymyr Zelensky Kharkiv
Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine akikaguwa hali ilivyo mjini Kharkiv.Picha: Ukrainian Presidential Press Office/AP Photo/picture alliance

Gavana huyo aliongeza kwamba shambulio hilo la siku ya Jumanne (Aprili 30) liliharibu jengo la makaazi ya watu, lakini huduma za dharura zilikuwa zikiendelea kama kawaida.

Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu (IRC) katika taarifa yake ilisema kwamba hali katika mji wa Kharkiv inazidi kuzorota huku wasiwasi ukiongezeka miongoni mwa wakaazi kufuatia mashambulizi ya anga ya mara kwa mara kutoka Urusi.

Soma zaidi: Zelensky: Ukraine imepata mafanikio katika utengenezaji wa makombora

Taarifa hiyo imeongeza kuwa mashambulizi ya hivi karibuni yamesababisha "uharibifu mkubwa wa miundombinu ya kiraia."

Urusi mara zote imekuwa ikikanusha kuwalenga raia katika vita hivyo ambavyo sasa vinaingia mwaka wake wa tatu.