SiasaUkraine
Mashambulizi ya makombora ya Urusi yawaua watu 3 Ukraine
30 Januari 2023Matangazo
Maafisa wa Ukraine wamesema mbali ya watu 3 waliouwawa, wengine 6 wamejeruhiwa katika hujuma hizozilizoulenga mji wa Kherson na ambazo zimesababisha pia uharibifu wa jengo la shule na hospital kwenye eneo hilo.
Soma pia:Zelensky: 2023 utakuwa mwaka wa ushindi kwa Ukraine
Kupitia hotuba ya kila siku kwa taifa rais Volodymyr Zelenskiy amesema Ukraine inapitia kipindi kigumu huko Donetsk na inahitaji msaada wa haraka wa silaha na aina mpya ya zana za kivita.
Amesema miji ya Bakhmut, Vuhledar na maeneo mingine ya mkoa wa Donetsk yanashuhudia mashambulizi makali ya Urusi anayoituhumu kuwa na malengo la "kuwafadhaisha na kuwavunja nguvu wapiganaji wa Ukraine"