Mashambulizi ya kigaidi yanamsaidia Trump
20 Septemba 2016Katika nyakati za kawaida, ushirikiano kati ya polisi na shirika la upelelezi wa ndani la FBI ungesherehekewa. Chini ya masaa 24 baada ya mashambulizi ya mabomu kati miji ya New Jersey na New York, mshukiwa mkuu wamashambulizi hayo si tu alitambuliwa, bali pia alikamatwa - na juu ya hayo, alijeruhiwa kifogo wakati wa kukamatwa kwake.
Ukweli kwamba tukio hilo lilipata usikivu mdogo wa vyombo vya habari - kama ilivyo kwa kila kitu wiki hii - unatokana na sababu moja: Donald Trump. Kwa mara nyingine tean, mgombea huyo wa chama cha Republican alikuwa na jibu rahisi kwa hofu ya Wamrekani kuhusiana na mashambulizi zaidi kutoka kwa Waislamu wenye itikadi kali nchini mwao: Ufuatiliaji kwa misingi ya rangi badala ya usahihi wa kisiasa.
Ukweli kwamba kitendo hicho kimepigwa marufu nchini Marekani unamhusu kidogo Trump - ni kinyume cha hilo. Kila wakati mmoja ya mawazo yake yanaenda kinyume na sheria, hiyo inakuwa sababu kwake na kwa wafuasi wake kuonesha ni namna gani mfumo ulivyooza, kuvunjika na kuharibika. Ni mtu wa nje ya mfumo wa kisiasa anaeweza kuhakikisha kuwa sheria zinawekwa kando kwa ajili ya lengo kuu, ambalo ni usalama wa nchi yake.
Suluhisho la mara moja
Uchambuzi mgumu kutoka kwa Hillary Clinton haukupokelewa vyema sana. Watu wengi hawataki kusikia namna vita vinavyoendelea mbali nchini Syria au Iraq vinahusishwa na Waislamu waliojazwa itikadi kali katika nchi yao. Hawana uhakika. Wana hofu. Wanataka suluhisho mara moja. Watu hawataki kukubaliana na athari za muda wa kati na mrefu.
Hakuna nafasi ya maswali ya nini kinafanya kwa jamii ambayo inajitambulisha kwa kutofautisha na mapambano dhidi ya ugaidi, na imezongwa na hofu na mashaka. Lakini madai kwamba umetosheka na unaweza kuondoa marufuku kwa sababu ya hofu yanafanana na madai ya chama cha itikadi kali za mrengo wa kulia cha Ujerumani cha AfD ya kwamba "Utaruhusiwa kusema hivyo."
Ni wazi kwamba Marekani haijapata njia ya kushughulikia namna sehemu ya raia wake wanavyoendeshwa na hisia za vitisho. Namna majadiliano yanavyoandaliwa inategemea sheria, lakini licha ya hayo raia wanahisi wanataka kuwa wakweli na hisia zao, wasiwasi na matumaini. Wengi wanaonekeana bado hawajakuja na njia za kushughulikia hofu zao na mashaka juu ya tabia za kibaguzi na chuki dhidi ya wageni.
Wasomi wamedhoofishwa
Na taifa hilo bado halijapata jibu mpaka wakati huu kwa swali la nguvu zipi za kiijamii ziko imara vya kutosha kuzuwia mgogoro kuo kushindwa kudhibitiwa. kilichowazi ni kwamba si wasomi wala vyombo vya habari wanaweza kutimiza jukumu hili. Hiyo ndiyo migogoro ambayo Marekani na nchi nyingine kama Ufaransa, Uingereza, Poland na sasa Ujerumani, zinakabiliana nayo. Lakini pia kuna maswali kwamba Marekani haipati muda katika joto inalokumbana nalo kwa sasa.
Marekani imepigika sana na kugawanyika baada ya kampeni ya miezi kadhaa ambayo inaonekana kusambaratika mbele ya kamera na kwenye mtandao wa twitter. Kwa uchaguzi huu imechelewa mno kujaribu kuanzisha mapambano juu ya namna ya kushughulikia miiko na msimamo wa kimaadili ambao nchi hiyo inataka kuwa nao. Wanasiasa katika mataifa mengine, wanakabiliwa na uchaguzi mkubwa katika muda mfupi, kuondoka katika maeneo yao ya kuridhika na kuingia katika uhalisia, ambako watu hali wanaishi.
Mwandishi: Ines Pohl
Mtayarishaji: Iddi Ssessanga
Mhariri: Mohammed Khelef