Mashambulizi ya bomu yaua watu 6 Nigeria
17 Juni 2011Matangazo
Katika shambulizi moja la kujitoa mhanga, bomu liliripuliwa katika gari mbele ya makao makuu ya polisi katika mji mkuu Abuja. Watu 2 waliuawa katika shambulio hilo na lilisababisha magari kadhaa kushika moto.
Saa chache baadae, bomu jingine liliripuka karibu ya kanisa katika mji wa Damboa ulio katika jimbo la Borno kaskazini-mashariki ya Nigeria. Kwa mujibu wa polisi, vijana 4 waliuawa na mtu mmoja alijeruhiwa.
Kundi la madhehebu ya Boko Haram lenye itikadi kali za Kiislamu limedai kuwa ndio lililohusika na shambulio la Abuja.