Mashambulizi ya anga ya Israel dhidi Gaza yaendelea
12 Mei 2023Matangazo
Mamlaka zimearifu kwamba mpaka sasa wapalestina 30 wameuwawa huku wasuluhishi kutoka nje wakiendelea na juhudi za kufanikisha kupatikana makubaliano ya kusitisha vita.
Soma zaidi:Umoja wa Mataifa walaani mauwaji ya raia Gaza
Jeshi la Israel jana lilisema kwamba baada ya kundi la wanamgambo wa Kipalestina la Islamic Jihad kufyetuwa maroketi ya masafa marefu katika ardhi ya Israel na kusababisha kifo cha mtu mmoja, ndege zake za kivita ziliwashambulia wanamgambo hao wanaofyatua makombora. Hata hivyo wakaazi wa Gaza wameripoti kutokea miripuko kwenye mashamba karibu na mji wa kusini wa Rafah. Hakuna ripoti zilizotolewa mara moja kuhusu vifo. Licha ya mashambulio hayo ya anga ya Israel hii leo asubuhi hali iliripotiwa kuwa ya utulivu.