Kama ulivyosikia hapo Baraza la Habari nchini Kenya limeelezea masikitiko yake juu ya kushambuliwa kinyama kwa waandishi habari kunakodaiwa kufanywa na polisi, wakati wa maandamano makubwa yaliyopangwa na upinzani. Kennedy Wandera ni mwenyekiti wa Muungano wa Wanahabari wa Idhaa za Kimataifa Afrika - FPAA