Mashambulio mjini Kabul
30 Novemba 2008Matangazo
Kabul:
Mtu mmoja amejiripua karibu na gari ya ubalozi wa Ujerumani katika mji mkuu wa Afghanistan-Kabul.Wizara ya mambo ya nchi za nje imesema mjini Berlin,mtumishi mmoja wa kiafghani aliyekua akiendesha gari hiyo amejeruhiwa.Shambulio hilo limegharim u maisha ya raia wawili wa Afghanistan.Wengi watatu wamejeruhiwa.Mtu huyo aliyevaa miripuko amejiripua kaariibu na shule katika njia kuu inayoelekea katika jengo la bunge la Afghanistan.Hili ni shambulio la nne dhidi ya Ujerumani katika kipindi cha wiki mbili.