1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mashambaulizi mapya yauwa watu 34 Gaza

29 Agosti 2024

Wapalaestina katika Ukanda wa Gaza wanasubiria usitishaji vita ili kuruhusu kampeni ya kutoa chanjo ya polio, huku mashambulizi yakizidi kurindima kwenye ukanda huo na kusababisha vifo vya watu wasiopungua 34.

https://p.dw.com/p/4k47b
Hospitali ya Al-Aqsa Gaza / Agosti 26, 2024
Wapalestina waliokimbia makazi yao wakiondoka kwenye eneo la Hospitali ya Mashahidi ya Al-Aqsa huko Deir al-Balah katikati mwa Ukanda wa Gaza kufuatia amri mpya ya Israeli ya kuondoka katika eneo hilo Agosti 26, 2024.Picha: Eyad Baba/AFPGetty Images

Umoja wa Mataifa unajiandaa kutoa chanjo kwa watoto wapatao 640,000 huko Gaza, ambako shirika la afya duniani WHO lilithibitisha kwamba alau motot mmoja ameathiriwa na ugonjwa huo wa kupooza. Umojawa Ulaya pia umetoa wito wa usitishaji vita kupisha kampeni hiyo.

Nukuu ya kauli ya pamoja kwa Umoja wa Ulaya inasema "Inatisha kwamba virusi vya polio vimegunduliwa na kwamba maambukizi ya mwanzo yamethibitishwa huko kwa mara nyingine mwezi Julai na kuwaathiri watoto."

Juhudi zadi zinahitaji katika usitishwaji wa mapigano huko Gaza

Mataifa ya Umoja wa Ulaya kwa pamoja yametoa rai kwa Umoja wa Mataifa na Shirika la Afya Duniani WHO kupigia chapuo hatua hiyo kwa haraka ili kufanikisha chanjo ya polio kwa watoto. Nchi 27 za Umoja wa Ulaya pia zimekaribisha hatua ya  uwasilishaji wa zaidi ya chanjo milioni 1.2 za  polio pamoja na ushirikiano wa Israeli katika utoaji chanjo hizo huko Gaza.

Katika hatua nyingine  kiongozi wa upinzani wa Israel, Yair Lapid amekataa madai yaliyotolewa na Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu kwamba kiongozi wa Israel hakupata onyo la mapema kuhusu shambulizi la Hamas. Lapid ameliambia gazeti la Jerusalem Post  la Alhamis hii kwamba Netanyahu alipewa taarifa, na yeye mwenyewe aliarifiwa, na taarifa hiyo ilitolewa kwa baraza la mawaziri.

Soma zaidi: Wito wa vita kusitishwa Gaza kupisha chanjo ya polio

Wasiwasi kuhusu mlipuko wa polio katika Ukanda wa Gaza
Mwanamke wa Kipalestina akimpa maziwa mtoto katika Hospitali ya Martyrs ya Al-Aqsa, huko Deir Al-Balah huko gaza Agosti 18, 2024.Picha: Ramadan Abed/REUTERS

Nukuu yake inasema " Ni kweli taarifa ilitolewa, Nilipewa taarifa," na kuongeza kuwa aliweza kuona taarifa za kijasusi za taifa, ambazo pia ziliweza kushuhudiwa pia na waziri mkuu na waziri mwenye dhima na baraza la mawaziri." Ilikuwa wazi kabisa kufahamu kile ambacho Hamas walikikusudia."

Lapid alisema alihudhuria mkutano wa usalama Agosti 21, 2023, na Netanyahu na mshauri wa kijeshi Meja Jenerali Avi Gil ambaye alionya kuhusu kile ambacho kilipewa jina la "mhimili wa upinzani" wa Iran  katika maeneo ya huko Lebanon,

Gaza na Ukingo wa Magharibi.

Amesema alidhani habari hiyo ilikuwa "isiyo ya kawaida" lakini kwake Netanyahu "alionekana kutokuwa na hamasa na kutojali na onyo hilo, kwa hivyo hakutowa maoni yoyote. Hata hivyo chama cha Netanyahucha mrengo wa kulia cha Likud kimemjibu Lapid kwa kusema kiongozi huyo anaongopa tena.

Kimesema kuwa Netanyahu hawakupata onyo lolote kabla ya Oktoba 7, wakati Hamas ilipovamia Israel, na kuua baadhi ya 1,200 na kuchukua mateka wapatao 250.